WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 20 March 2015

USALAMA WETU

Usalama Wetu
Ulinzi Jirani
Ulinzi Jirani ni nini?
·       Ni mpango wa wananchi wa eneo la makazi kwa hiari yao wanaamua kushirikiana kujilinda wao na mali zao dhidi ya vitendo vya uhalifu kwa kuwa na mpango wa kupeana taarifa za kiusalama hivyo kufanya kuwepo na mtandao wa ulinzi jirani miongoni mwao.
·       Mpango unalenga kuzuia uhalifu na unapotokea kuufuatilia kwa karibu.
·       Mpango unawataka majirani kujiunga na kushirikiana katika mipango na mikakati ya kujihakikishia usalama wao na mali zao.
·       Wakazi wa eneo husika wanashauriwa kujiunga katika vikundi vidogovidogo vya ulinzi wa makazi yao.
·       Jeshi la Polisi linachangia utaalamu na ushauri kwa vikundi hivyo vya ulinzi juu ya masuala ya ulinzi na usalama.
·       Wananchi na Jeshi la Polisi kwa pamoja wana jukumu la kuufanya mpango wa ulinzi jirani kuwa endelevu na wa kudumu.

OKOA MAISHA NA MALI


No comments:

Post a Comment