USALAMA WETU
JUKUMU LA
WANANCHI KATIKA MPANGO WA ULINZI JIRANI
Majukumu
ya Msingi ya Wananchi katika Mpango wa Ulinzi Jirani:
· Kuwa macho
na masikio ya masuala ya ulinzi na usalama katika eneo lao.
· Wananchi
wana jukumu la kushirikiana na Polisi katika kutafuta ufumbuzi endelevu wa
matatizo ya kiusalama yanayojitokeza ndani ya jamii yao.
· Kwa
pamoja watapanga mipango inayotekelezeka ya kujihakikishia usalama wa maisha na
mali.
· Ulinzi jirani ni moja ya mipango
inayotekelezeka kirahisi na bila gharama.
Kama
mpango wa Ulinzi Jirani utapangwa vema na kutekelezwa kwa ushirikiano mzuri wa
wananchi na Jeshi la Polisi, mambo makuu yatajitokeza katika jamii:
· Makazi ya wananchi yatakuwa salama na
yenye amani na utulivu kwa kuwa wahalifu watatokomea.
· Ushirikiano baina ya wananchi na Jeshi
la Polisi utakuwa wa karibu na utaimarika hivyo uhalifu utadhibitiwa.
No comments:
Post a Comment