JINSI YA KUTAMBUA VITENDO VYENYE KULETA SHAKA YA UHALIFU
·
Ni muhimu kuwa macho wakati wowote kwa jambo
lolote linalotendeka nje ya utaratibu. Kwa mfano, tendo linafanyika muda ambao
sio wa kawaida kama vile usiku au mahali ambapo sio pa kawaida kwenye kificho. Tendo kama hilo linaweza kuashiria uhalifu.
·
Kuwepo kwa mtu au watu wasio wakazi wa eneo,
wanaopitapita mtaani bila sababu maalumu.
·
Kuwepo kwa milango au madirisha yaliyo wazi
au kuvunjwa katika eneo ambapo daima huwa limefungwa au nyumba ambayo haina
watu. Hii inaweza kuwa ashirio la tendo la uvunjaji wa nyumba.
·
Kuwepo kwa karakana za kificho kunaweza
kuashiria ni mahali maalumu pa kubadili alama, namba au umbile la chombo
kilichoibiwa.
·
Kusikia sauti au kelele ambazo sio za kawaida
kama vile mlio wa bunduki, kupiga yowe, au mbwa kubweka kwa muda mrefu. Hili linaweza kuwa ashirio la kutendeka tendo
la uhalifu.
·
Mtu kuonyesha ishara za kiakili au kimwili
ambazo sio za kawaida. Inawezekana mtu
akawa ameumizwa, ana athari za madawa ya kulevya au anahitji msaada wa matibabu.
VITENDO
KAMA HIVI VINAPOONEKANA KATIKA ENEO LAKO WAJULISHE MAJIRANI NA TOA TAARIFA KATIKA SERIKALI YA
MTAA AU POLISI KWA KUTUMIA SIMU YA DHARURA.
No comments:
Post a Comment