Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kulia), Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir (wanne kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu, Hamisa Kalombola (watatu kushoto) pamoja na Viongozi na Wanaharakati wa Taasisi ya Imetosha inayopambana na kutokomeza mauaji ya watu wenye ualbino nchini wakiimba wimbo wa Tanzania Nakupenda katika viwanja vya Leaders Club mara baada ya kufanya Matembezi ya Hisani yaliyoanzia viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo yaliandaliwa na Taasisi hiyo kwa kuwashirikisha mamia ya washariki kutoka katika vikundi mbalimbali vya mazoezi ya viungo jijini Dar es Salaam pamoja na wageni waalikwa.
Mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba yake yenye kulaani mauaji
ya albino nchini mbele ya viongozi na wanaharakati wa Taasisi ya Imetosha inayopambana
na kutokomeza mauaji ya watu wenye ualbino nchini pamoja na mamia ya washiriki
wa Matembezi ya Hisani (hawapo pichani). Katika hotuba yake, Chikawe aliwaomba
wananchi washirikiane na serikali kikamilifu katika kuwalinda watu wenye ualbino
ili kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea hasa katika mikoa ya Kanda ya
Ziwa. Hata hivyo, Chikawe alisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwakamata
watuhumiwa pamoja na kutoa ulinzi mkali kwa albino, pia alisema Serikali
itashirikiana na Taasisi hiyo ili kuendelea kupinga ukatili huo wanaotendewa
albino. Waziri Chikawe alisema hayo baada ya kushiriki matembezi hayo
yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders Club jijini Dar
es Salaam leo.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar
Kweigyir (watatu kushoto), washiriki wa Matembezi ya Hisani ya kupinga mauaji
ya albino wakishangilia mara baada ya kufanya matembezi hayo
yaliyoandaliwa na Viongozi na Wanaharakati wa Taasisi ya Imetosha inayopambana
na kutokomeza mauaji ya watu wenye ualbino nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), aliyaongoza matembezi hayo yaliyoanzia
viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam leo
na kuwaomba wananchi washirikiane na Serikali kuwalinda watu wenye ualbino ili
kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea nchini.
Balozi wa Taasisi ya Imetosha
ambaye pia ndiye mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Henry Mdimu akitoa hotuba yake
fupi kwa mgeni rasmi pamoja na mamia ya washiriki (hawapo pichani) wa matembezi
ya hisani ambayo yaliandaliwa na taasisi hiyo ikiwa ni Kampeni Maalum ya
kupinga mauaji ya albino nchini. Kwa mujibu wa Mdimu, taasisi yake inatarajia
kwenda katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kutoa elimu kwa wananchi hao kuhusiana
na imani potofu dhidi ya mauaji ya albino.
Sehemu ya washiriki wa Matembezi ya
Hisani ya kupinga mauaji ya albino nchini wakifanya mazoezi ya viungo baada ya
kufanya matembezi hayo yaliyoandaliwa na Viongozi na Wanaharakati wa Taasisi ya
Imetosha inayopambana na kutokomeza mauaji ya watu wenye ualbino nchini. Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), aliyaongoza
matembezi hayo yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders
Club jijini Dar es Salaam na kuwaomba wananchi washirikiane na Serikali kuwalinda
watu wenye ualbino ili kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea nchini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Imetosha, Masoud
Kipanya (kulia) akielezea jinsi yeye pamoja na Balozi wa Taasisi hiyo, Henry
Mdimu (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa taasisi hiyo, walivyopania
kuhakikisha wanasambaratisha mauaji ya albino nchini. Taasisi hiyo imefanya matembezi
ya hisani ikiwa ni kampeni maalum ya kupinga mauaji ya albino nchini. Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), aliyaongoza matembezi
hayo yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders Club jijini
Dar es Salaam na kuwaomba wananchi washirikiane na Serikali kuwalinda watu
wenye ualbino ili kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea nchini.
No comments:
Post a Comment