Afisa Operesheni wa Idara ya Wakimbizi, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Stephen Daniel (kushoto) akiwaelekeza raia wapya wa
Tanzania katika Kijiji cha Ilangu, Makazi ya Mishamo, kuwasilisha vyeti vya kliniki
vya watoto wao ili waweze watoto wao kuwekwa kwenye kumbukumbu ya Serikali.
Watoto wote waliozaliwa baada ya mwaka 2010 ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa, hivyo
hawatapewa vyeti vya uraia kama wanavyopewa wazazi wao. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa
wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia
wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha
zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya
Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la
Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. |
No comments:
Post a Comment