Raia wapya wa Tanzania, wakazi wa Kijiji cha
Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Shukuru Nzokila (kulia) na Anicet
Yohanna wakishangilia baada ya kupokea vyeti vyao vya uraia wa Tanzania, katika
Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa
wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia
wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari
wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa
Makazi ya Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika
la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. |
No comments:
Post a Comment