WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 26 June 2015

NAIBU WAZIRI SILIMA AKABIDHI MSAADA WA GARI KWA JESHI LA POLISI ILI LIWEZE KUTUMIKA KUTOA ELIMU KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WA BARABARA NCHINI


Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Naibu Waziri Wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame  Silima (Kulia), akimkabidhi funguo ya gari Naibu Kamanda wa Polisi (IGP), Abdallah Kaniki ikiwa ni msaada uliotolewa kwa Jeshi la Polisi, gari hilo limetolewa kwa madhumuni ya kutoa elimu na tahadhari kwa madereva na watumiaji wa barabara huku tukienda kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani. Msaada huo ulitolewa jana katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ,jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Naibu Waziri Wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, akilikagua gari muda mfupi kabla ya kulikabidhi kwa Jeshi la Polisi, gari hilo limetolewa kwa madhumuni ya kutoa elimu na tahadhari kwa madereva na watumiaji wa barabara huku tukienda kuadhimisha Wiki   ya Nenda kwa Usalama barabarani,.msaada huo ulitolewa jana katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
 

Naibu Kamanda wa Polisi (IGP), Abdallah Kaniki (kushoto), akimshukuru Naibu Waziri Wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwa msaada wa gari lililotolewa na na Baraza hilo kwa Jeshi la Polisi nchini. Msaada huo ulitolewa jana katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.


Naibu Kamanda wa Polisi nchini (IGP), Abdallah Kaniki (kushoto), akimshukuru mmoja wa wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani baada ya kukabidhiwa gari lililotolewa na Baraza hilo. Hafla hiyo ilifanyikia Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, jijini Dar es Salaam.


Naibu Kamanda wa Polisi (IGP), Abdallah Kaniki (kulia), akionyesha funguo ya gari walilokabidhiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, ambae pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kwa msaada wa gari lililotolewa na Baraza hilo,jijni Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi  cha Usalama Barabarani Nchini, Naibu Kamishna  Mohamed Mpinga. Hafla hiyo ilifanyikia Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment