WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 23 June 2015

RAIS KIKWETE AMTUNUKU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MBARAK ABDULWAKIL NISHANI YA UTUMISHI MREFU NA MAADILI MEMA DARAJA LA (I)

Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, baada ya kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Ernest Mangu (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete, katika sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) John Minja (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete, katika sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete, katika sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika Ukumbi Mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtunukia Katibu Mkuu huyo, Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I).  
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) John Minja (kulia) na Mkurugenzi wa Sera na Mipango, wa Wizara hiyo, Haji Janabi, nje ya Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtunuku Katibu Mkuu huyo, Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I). 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kushoto) akiwa na baadhi ya Watunukiwa wakiwa katika hafla hiyo wakati wakisubiri kutunukiwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kwenda nyuma mstari wa kwanza) akiwa na baadhi ya Watunukiwa wakiwa katika hafla hiyo wakati wakisubiri kutunukiwa. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.

Rais Jakaya Kikwete (wanne kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Watunukiwa wa Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la Kwanza. Wakwanza kulia mstari wa nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  

No comments:

Post a Comment