WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday 2 June 2015

SILIMA AZINDUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA VITAMBULISHO VYA TAIFA VYA KIELEKTRONIKI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akikata utepe kuzindua mkutano wa Kimataifa kuhusu Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki, ulioanza leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena. Kulia kwa Naibu Waziri ni Waziri wa Maendeleo na Mshikamano wa  Jamii  wa Jamhuri ya Djibout, Zahar Youssuouf Kayad, na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hapa nchini, Joseph Makani na kushoto ni Naibu Waziri wa Mawasiliano wa Ghana, Bw. Edward Ato Sarpong, na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Asia Pacific Smart Card Association, Bw. Greg Pote.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, akihutubia  katika mkutano wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika, ulioanza leo Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.  Mbele yake ni wageni toka mataifa mbalimbali  wanaohudhuria mkutano huo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maofisa wa moja ya makampuni yanayoshiriki katika mkutano wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika unaoendelea Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akipata maelezo kutoka kwa moja ya makampuni yanayoshiriki mkutano wa Kimataifa wa  Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika unaoendelea Jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.

Mmoja wa washiriki wa Maonyesho kuhusu Vitambulisho vya Kielektroniki yanayoendelea katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, Cyrille Volentier  akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima kuhusu shughuli zinazofanywa na Kampuni yake inayojishughulisha na uchapishaji wa vitambulisho vya kielektroniki.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) na  Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Joseph Makani wakifuatilia mada katika  mkutano wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika unaofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika mkutano  wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika unaoendelea katika Hoteli ya Serena.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka nchi mbalimbali wanaohudhuria  mkutano wa Kimataifa wa Vitambulisho vya Taifa vya Kielektroniki Barani Afrika unaoendelea katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment