WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 2 June 2015

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WASHIRIKI KIKAO KAZI CHA UTAYARISHAJI WA MPANGO WA MANUNUZI WA WIZARA WA MWAKA 2015/2016 MJINI MOROGORO

Sehemu ya wajumbe wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo  ya Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016  kinachowahusisha Maafisa Bajeti, Manunuzi, Wakurugezi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Taasisi zote za wizara hiyo kilichoanza leo katika Hoteli ya Oasisi mjini Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (katikati-waliokaa)  akiwa pamoja na Wakuu wa Taasisi zote za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi waliohudhuria Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa wizara wa mwaka 2015/2016 kilichoanza leo katika Hoteli ya Oasis mjini Morogoro. Watatu kutoka kushoto ni Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve na wapili kushoto ni Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga, waliosimama nyuma ni baadhi ya Wakurugenzi Wasaidizi wa wizara, Maafisa Bajeti pamoja na Maafisa Ununuzi wa wizara.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akisalimiana na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edwin Makene (kulia) baada ya kupokelewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi cha wizara hiyo, Manyama Mapesi akielekea kufungua Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa wizara wa mwaka 2015/2016 kilichoanza leo katika Hoteli ya Oasis mjini Morogoro.

Kamishna wa Lojistiki na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Wajumbe wote wa Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka 2015/2016, baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) kufungua Kikao Kazi hicho katika Hoteli ya Oasisi mjini Morogoro. wa Kushoto ni Mkurugenzi wa Manunizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Manyama Mapesi.

No comments:

Post a Comment