WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 22 June 2015

WASANII MAARUFU WA VICHEKESHO WA KUNDI LA KASHI-KASHI WATEMBELEA BANDA LA MAONYESHO LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

   “UTII WA SHERIA BILA SHURUTI” Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Jesca Kindole (Safina) akipigia saluti sanamu la askari wa Jeshi la Polisi wa kipindi cha kikoloni, wakati  msanii huyo na wenzake walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

     Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, wakipewa maelezo na Koplo wa Jeshi la Polisi, Sylvester Mganga, kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Jesca Kindole (Safina), Habib Mrisho (Sumaku), na Rashid Costa (Maringo 7).

  Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba (kulia) akiwapa maelezo wasanii maarufu wa vichekesho wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, kuhusu taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na Jeshi hilo, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


      Msanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi anayeshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Habib Mrisho (Sumaku) akisaini kitabu cha wageni katika banda la Jeshi la Magereza wakati msanii huyo na mwenzake Jesca Kindole kwa jina maarufu la uigizaji (Safina) walipotembelea mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kulia ni maafisa wa Jeshi hilo.

  Wasanii maarufu wa vichekesho nchini wa Kundi la Kashi-Kashi wanaoshiriki katika kipindi cha Mizengwe cha Kituo cha ITV, Habib Mrisho (Sumaku) na Jesca Kindole (Safina), wakisoma Hati za Kusafiria zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji. Wasanii hao walitembelea Mabanda ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Idara hiyo, Tatu Burhan.

No comments:

Post a Comment