WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 6 July 2015

WAZIRI CHIKAWE ATANGAZA MAFANIKIO YA WIZARA YAKE KATIKA KIPINDI CHA MIAKA KUMI YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne. Chikawe alisema kupitia taasisi zake yakiwemo Majeshi ya Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Idara ya Wakimbizi pamoja na Idara zingine zilizoko chini ya wizara hiyo, imepata mafanikio makubwa hususani katika jukumu la msingi la ulinzi na usalama wa nchi jambo ambalo limewezesha nchi kuwa na amani na utulivu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne. Chikawe alisema kupitia taasisi zake yakiwemo Majeshi ya Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Idara ya Wakimbizi pamoja na Idara zingine zilizoko chini ya wizara hiyo, imepata mafanikio makubwa hususani katika jukumu la msingi la ulinzi na usalama wa nchi jambo ambalo limewezesha nchi kuwa na amani na utulivu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja.
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (D-IGP), Abdulharman Kaniki akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu uwepo wa vituo vidogo vya polisi nchini (Police Posts) pamoja na majukumu yake. Kwa mujibu wa D-IGP, vituo hivyo vipo kwa mujibu wa sheria na haviruhusiwi kuwa na silaha za moto, na endapo askari wa vituo hivyo vidogo wakimkamata mtuhumiwa watampeleka katika vituo vikubwa vya polisi ili utaratibu mwingine wa kisheria uweze kufanyika. Kiongozi huyo wa Polisi alipewa nafasi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu vituo hivyo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya wizara katika Serikali ya Awamu ya Nne, uliofanyika katika Ukumbi wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment