WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday 30 June 2015

WAZIRI CHIKAWE AZINDUA KIKOSI KAZI CHA KUPAMBANA NA UHALIFU WA KIMAZINGIRA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Katika hotuba yake IGP Mangu aliomba ushirikiano na wananchi katika kupambana na uharibifu  wa mazingira nchini. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.  Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.

Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Utunzaji wa Mazingira (ICCF) la nchini Marekani, Dk Kaush Arha akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali nchini pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana na uhalifu wa kimazingira kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu nchini. Uuzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu.
Viongozi mbalimbali wa Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. 
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment