WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 4 August 2015

NAIBU WAZIRI SILIMA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI JIJINI TANGA LEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini Malawi ambaye pia ni Kiongozi wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini humo, Maepheson Matowe.  Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo.

Sehemu ya Wadau na Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo .
Mtoa mada wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Usalama Barabarani ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samweli Manyele akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Prof. Manyele alitoa elimu ya jinsi ya kusafirisha salama kemikali. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo.

No comments:

Post a Comment