WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday 18 August 2015

NAIBU WAZIRI SILIMA AONGOZA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NA PEMBE YA AFRIKA KATIKA MAPAMBANO YA KUZUIA NA KUDHIBITI UZAGAAJI WA SILAHA HARAMU (RECSA), ZANZIBAR LEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuwakaribisha nchini wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kabla ya kufungua kikao cha wajumbe hao kinachofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar. Lengo la kikao hicho ni  kujadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania.
Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan ya Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) ndio Mwenyekiti wa Baraza hilo, hata hivyo katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia meza kuu) anamuwakilisha katika kikao hicho.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini, Pereira Ame Silima (kulia) akiwa na  Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Uganda ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi James Baba (katikati) na Mjumbe wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani nchini Rwanda, Balozi Munyabagisha Valeus, wakisoma taarifa za masuala mbalimbali ya jinsi ya Kupambana ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Baraza hilo limekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi nchini, Pereira Ame Silima (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo ambalo nchi zake wanachama ni Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Wajumbe hao wamekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo. Picha zote Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment