Daktari Hafidh Ameir toka Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) akitoa elimu juu ya umuhimu wa kupima afya
kwa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Semina iliyofanyika
Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Marcelina Henry akichukuliwa vipimo vya shinikizo la damu na Muuguzi toka
Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Asma Msimbe wakati wa zoezi la kupima
afya kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Bwana Ponela John wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi akichukuliwa vipimo vya urefu na Bwana John Joseph wa Timu ya Wataalamu
waliofika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kupima afya za
wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
1. Mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Bi. Radhia Said akichukuliwa vipimo vya urefu na Bwana John Joseph wa
Timu ya Wataalamu waliofika Wizara hapo kwa ajili ya kuendesha zoezi la kupima
afya za wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment