WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday, 19 August 2015

SEKRETARIETI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU YATOA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI

 Afisa Mwandamizi kutoka Sekretarieti ya kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Alex Lupiya akitoa mada kuhusu Dhana ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu wakati wa semina kwa waandishi wa vyombo vya habari nchini iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jijini Dar es Salaam.

 Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora, Joshua Taramo akitoa mada kuhusu Mikakati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu wakati wa semina kwa waandishi wa vyombo vya habari nchini iliyofanyika makao makuu ya Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi Jijini Dar es Salaam.

 Mwandishi wa Habari kutoka  kituo  cha Televisheni cha  Azam, Ismail Hamza,akiuliza maswali wakati wa semina kwa waandishi wa vyombo vya habari nchini iliyofanyika makao makuu yaWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakimsikiliza Msaidizi wa mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, John Makuli (hayupo pichani), wakati akiwasilisha mada kwenye semina kwa Waandishi wa vyombo vyahabari nchini iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment