WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday 29 September 2015

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI ATEMBELEA KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU ILIYOKO WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA NA KUWATAKA WAKIMBIZI HAO WADUMISHE AMANI NA UTULIVU

Mkurugenzi  wa  Idara  ya Wakimbizi  kutoka  Wizara    ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (kushoto) akizungumza  na watumishi wa mashirika  mbalimbali yaliyoko katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) aliyetembelea kambi hiyo jana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akizungumza na watumishi mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo inahifadhi wakimbizi  kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Daktari wa Hospitali ya Kambi ya Wakimbizi ya  Nyarugusu, Florence Mshana(aliyeshika karatasi), akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(kushoto),  alipotembelea hospitali hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo inahifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Amah Assiama-Hillgartner( kushoto),  akitoa maelezo kwa Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani,  Mbarak Abdulwakil(katikati),  aliyetembelea hospitali  hospitali hiyo wakati wa ziara yake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akiongozana na Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B), Fredrick Nisajile (kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kambini hapo jana. Kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma inahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwaki l(katikati), akiongozana na Mkuu wa Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu (B), Fredrick Nisajile (kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu katika  makazi ya wakimbizi  yaliyopo Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akimsikiliza mmoja wa maofisa wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) alipotembelea ndani ya mahema wanakoishi wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.


No comments:

Post a Comment