WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 29 September 2015

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA KAMBI ZA NDUTA,MTENDELI NA KARAGO ZILIZOPO KATIKA MPANGO WA KUPOKEA WAKIMBIZI WALIOHIFADHIWA KWA MUDA KAMBINI NYARUGUSU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(shati jeupe), akimsikiliza mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner, wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya Mtendeli, Nduta na Karago ambayo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakishirikiana na mashirika ya kuhudumia wakimbizi wamepanga kuhamishia wakimbizi kutoka nchini Burundi baada ya kuhifadhiwa kwa muda kambini Nyarugusu, wliayani Kasulu, mkoani Kigoma.Kushoto ni mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B), Fredrick Nisajile.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(shati jeupe),akisoma maandishi yaliyoandikwa katika ubao wa moja ya madarasa yaliyokuwa yakitumiwa na watoto wa wakimbizi katika kambi ya Nduta.Kambi hiyo ni mojawapo ya makambi ambayo wakimbizi waliohifadhiwa kwa muda kambini Nyarugusu watahamishiwa hapo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akitoka kukagua moja ya madarasa katika kambi ya wakimbizi ya Mtendeli, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakishirikiana na mashirika ya kuhudumia wakimbizi wamepanga kuhamishia wakimbizi kutoka nchini Burundi baada ya kuhifadhiwa kwa muda kambini Nyarugusu, wliayani Kasulu, mkoani Kigoma.anayefuatia ni mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B), Fredrick Nisajile.
Baadhi ya nyumba zitazotumiwa na wakimbizi watakaohamishiwa kambini hapo wakitokea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu huku ukiwa ni mpango wa serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakishirikiana na mashirika ya kuhudumia wakimbizi wamepanga kuhamishia wakimbizi kutoka nchini Burundi baada ya kuhifadhiwa kwa muda kambini Nyarugusu, wliayani Kasulu, mkoani.
Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B), Fredrick Nisajile (kulia), akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(katikati),wakati wa ziara hiyo.kushoto ni mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner.
Afisa wa Shirika la Chakula Duniani(WFP),Michael Bisama akitoa maelezo  mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mbarak Abdulwakil (shati nyeupe) na ujumbe wake, kuhusiana na ujenzi wa hema la kuhifadhia chakula katika kambi mpya ya Nduta ambayo iko katika mpango serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakishirikiana na mashirika ya kuhudumia wakimbizi wamepanga kuhamishia wakimbizi kutoka nchini Burundi baada ya kuhifadhiwa kwa muda kambini Nyarugusu, wliayani Kasulu, mkoani.


No comments:

Post a Comment