WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 29 September 2015

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI NA WADAU MBALIMBALI WANAOSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTOA HUDUMA KATIKA KAMBI ZA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi wa Programu kutoka Shirika la World Church Service, Sarah Krause(kushoto),shirika hilo linashirikiana na Serikali kutoa huduma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma,Katibu Mkuu alikutana kwa chakula cha jioni na wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Serikali katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma.Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi,Harrison Mseke, hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR) wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Mwakilishi wa Shirika la OXFAM kutoka nchini Ireland ,Michael O’ Riordan akizungumza wakati wa chakula cha jioni kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani,Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani), hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR) wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mkuu wa Operesheni katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu,OC Lusesa ,akizungumza wakati wa chakula cha jioni kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani,Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani), hafla hiyo ilifanyika jana  katika ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR) wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Baadhi ya wadau wanaoshirkiana na Serikali ya Tanzania katika kutoa huduma mbalimbali katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wakibadilishana mawazo jana  wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR) wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akiongoza wadau kuchukua chakula  jana wakati wa hafla iliyowashirikisha wadau wanaoshirikana na Serikali kutoa huduma katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma, hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR) wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akibadilishana mawazo na wadau mbalimbali wanaoshirikana na Serikali kutoa huduma katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma, hafla hiyo ilifanyika jana  katika ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR) wilayani Kasulu mkoani Kigoma.


No comments:

Post a Comment