WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 29 September 2015

PICHA MBALIMBALI ZA WANAFUNZI AMBAO NI WATOTO WA WAKIMBIZI WA SHULE YA MSINGI VUMILIA KATIKA KAMBI YA NYARUGUSU, KASULU MKOANI KIGOMA

Wanafunzi  wa Shule ya msingi Vumilia  ambao ni watoto wa  wakimbizi wa Burundi, wakiwa wamepanga mstari nje ya darasa lao jana muda mfupi kabla ya kuanza masomo, masomo shuleni hapo ufundishwa kwa kutumia mtaala wa Burundi.Huduma za elimu katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma hutolewa kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF).
Mwalimu Nijimo Jean wa shule ya msingi Vumilia iliyoko katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma, akiwafundisha wanafunzi wa darasa la pili  ambao ni watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi.elimu shuleni hapo hutolewa kwa kutumia mtaala wa Burundi.
 
Mwalimu Ciza Aline wa shule ya msingi Vumilia akiwafundisha wanafunzi wa darasa la kwanza ambao ni watoto wa wakimbizi wa Burundi ,shule hiyo iko katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Wanafunzi  wa darasa la pili wa  Shule ya msingi Vumilia  ambao ni watoto wa  wakimbizi wa Burundi wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kutoka darasani.


No comments:

Post a Comment