WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday 13 November 2015

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA IDARA YA UHAMIAJI KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM – AWATAKA WATENDAJI KWENDA NA KASI MPYA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja , wakati wa  ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini jijini Dar es Salaam.  Wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile (kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya Ofisi za Idara ya Uhamiaji, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),akipewa maelezo alipotembelea Dawati la Mapokezi wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,Kurasini, jijijni Dar es Salaam.
Afisa Uhamiaji, Lilian Maleko akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai), jinsi  taarifa za muombaji pasi ya kusafiria zinavyohakikiwa, wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa hati za  kusafiria,  Amir Hassan (wa pili kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),moja ya pasi iliyokua imeshachapwa tayari kwa matumizi ya kusafiria, wakati wa ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Uhamiaji (Vibali vya Ukaazi, Visa na Pasi), Victoria Lembeli (katikati), akimuonesha  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, moja ya karatasi iliyokataliwa na mfumo wa komputa baada ya kubainika kwa taarifa za uongo za muombaji wa Hati ya Ukaazi, wakati Naibu Katibu Mkuu  huyo alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Idara ya Uhamiaji, wakimsikiliza  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (hayupo pichani), alipofanya mkutano nao wakati wa ziara aliyofanya  Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Silvester Ambokile akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya machapisho ya Idara ya Uhamiaji, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai) katika picha ya pamoja na viongozi wa Idara ya Uhamiaji wakati alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.  Wa pili kushoto mstari wa mbele, ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bi. Lilian Mapfa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment