WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 13 November 2015

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA NA KUWATAKA KUIMARISHA MIRADI YA UZALISHAJI YA JESHI HILO

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja, akitoa taarifa ya Jeshi hilo wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, ( katikati) alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pancrass.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia), akipokea taarifa za Miradi inayoendeshwa na Jeshi la Magereza nchini kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Minja, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Maafisa wa Jeshi la Magereza (hawapo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijni Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo,( kulia), akiagana na Maafisa wa Jeshi la Magereza,baada ya kumaliza kutembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo ( wa tatu kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Jeshi la Magereza muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto waliokaa ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Minja.No comments:

Post a Comment