WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 13 November 2015

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NA KUWATAKA KUBUNI MIRADI MBALIMBALI YA KUONGEZA MAPATO NDANI YA JESHI HILO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo (Kushoto), akisalimiana na Maofisa  wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Braiton Manyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo katika mtaa wa Lumumba,jengo la Ushirika,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo katika mtaa wa Lumumba,jengo la Ushirika,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,ambaye pia ni Kamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali (kulia), akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, taarifa ya ujenzi la Jengo laa  linalotarajiwa kuwa Makao Makuu ya Jeshi hilo, alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizoko TAZARA ,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza  na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), alipotembelea Ofisi za Jeshi hilo zilizopo TAZARA ,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (wa tatu kutoka kulia waliokaa),akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji muda mfupi baada ya kumaliza ziara ya kutembelea makao Makuu ya Jeshi hilo na Ofisi zilizopo Tazara,jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment