Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza
na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali,
Pius Nyambacha (wapili kulia) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Makao Makuu
ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Rwegasira
alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi
zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba. Kulia ni Fikiri Salla, Kamishna wa Usalama
kwa Umma Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Kamishna wa Operesheni wa
Jeshi hilo, Rogatius Kipali (kushoto).
|
No comments:
Post a Comment