WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 15 January 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI AWAONYA WANAOCHAFUA SERIKALI KUHUSIANA NA OPERESHENI KAMATA WAHAMIAJI HARAMU

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akisalimiana na Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Haji Hamza wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Uhamiaji Zanzibar zilizopo katika eneo la Kilimani. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Visiwani Zanzibar waliokuwa wakisubiri huduma katika ofisi za Uhamiaji alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji zilizoko Kilimani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akikagua jarada lenye kuonyesha kumbukumbu za waombaji wa hati za kusafiria kutoka katika familia yake, aliyesimama ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu akifuatiwa na Naibu Kamishna wa Utawala na Fedha. Masauni alifanya ziara hiyo ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za kiutendaji.

Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu akitoa taarifa ya utendaji kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati) aliyefanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji katika ofisi za Uhamiaji zilizopo eneo la Kilimani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizungumza na watendaji wakuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar alipofanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji. Waziri huyo ametoa onyo kwa maafisa wote wanaotumia zoezi la kukamata wahamiaji haramu kinyume na agizo la serikali kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati waliokaa) pamoja na kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu (kulia-waliokaa) na kamishna wa Utawala na Fedha (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wengine wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, alipofanya ziara ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za kiutendaji idarani hapo. 


No comments:

Post a Comment