Kaimu
Balozi wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika sherehe ya raia wa China
wanaoishi nchini ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa
Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) kuja kuzungumza na
mamia ya wachina hao waliohudhuria sherehe hiyo. Katika hotuba yake, Waziri
Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri, wa miaka mingi uliopo
kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za
kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni
nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
|
No comments:
Post a Comment