WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Saturday 30 January 2016

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ASIFU MIRADI YA UFUGAJI GEREZA LA UZALISHAJI MIFUGO MTEGO WA SIMBA, KINGOLWIRA MKOANI MOROGORO

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, (kushoto) akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Magereza alipotembelea Gereza la uzalishaji mifugo Mtego wa Simba lililopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Gereza la uzalishaji mifugo Mtego wa Simba mkoani Morogoro. Kulia ni Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Omari Msepwa.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba, Constatus Magori akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa gerezani hapo mkoani Morogoro.
Kundi la ng’ombe wa maziwa wanaofugwa katika shamba la uzalishaji mifugo Gereza la Mtego wa Simba, Kingolwira mkoani Morogoro wakiwa malishoni kama wanavyoonekana katika picha.

Mtaalamu wa mifugo katika mradi wa ufugaji kuku wa mayai na nyama uliopo Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, lililopo Kingolwira mkoani Morogoro, Sajenti Sarah Kabunda (wapili kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) alipotembelea Gereza hilo Januari 30, 2016 kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji  zinazofanywa gerezani hapo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto), akiangalia moja ya mashuka yanayofumwa kwa ustadi mkubwa na wafungwa wa kike katika Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira mkoani Morogoro. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

No comments:

Post a Comment