Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin
Komba (wapili kushoto waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi-Makao Makuu,
Hezron Gyimbi (wapili kulia), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Yusuph
Ilembo (kulia) na kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na
Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha
Haramu (RECSA), Esaka Mugasa, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
Warsha ya Kuhamasisha Sheria Mpya ya Udhibiti wa Silaha na Risasi. Warsha hiyo
ya siku mbili ilifunguliwa na Katibu Mkuu, Rwegasira katika Ukumbi wa Bwalo la
Maafisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
|
Habari
ReplyDeleteNina jambo nahitaji kushauri
kama inawezekana, tunaomba kianzishwe kitengo cha PF3 katika hospitali zetu ili kuepusha vifo vinavyoweza kutokea kutokana na kuchelewa kupata PF3 kwa wakati.
Naamini kama miongozo itaruhusu, jambo hili la kuanzisha kitengo cha PF3 kwenye hospitali zetu laweza kuwa msaada.
Nawatakia kazi njema
mazigob@gmail.com