WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 22 February 2016

WAZIRI KITWANGA AFANYA KIKAO NA WATENDAJI WAKUU WA JESHI LA POLISI NA WAKUU WA IDARA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na wakwanza upande wa kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) akizungumza jambo katika kikao kazi alichokitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akizungumza jambo katika kikao kazi alichokitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Balozi Simba ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.Wakwanza upande wa kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) kuhusu masuala mbalimbali ya kikazi ndani ya Jeshi lake katika Kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoitishwa na Waziri Kitwanga na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akifuatiwa na Naibu wake, Balozi Simba Yahya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment