WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday, 2 March 2016

MAREKANI YAIKABIDHI SERIKALI YA TANZANIA MBWA MAALUMU WA KUBAINI DAWA ZA KULEVYA NA PEMBE ZA NDOVU

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akizungumza katika shughuli ambapo Marekani iliikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika shughuli hiyo.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser akizungumza katika shughuli ambapo nchi yake iliikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe,wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni, anayefuata ni  Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika shughuli hiyo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akimuaga Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser mara baada ya Marekani kuikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Usalama Kanda, Ubalozi wa Marekani nchini, Bruce Paluch.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akiwafafanulia jambo waandishi wa habari mara baada ya Serikali ya Marekani kuikabidhi Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (D/IGP), Abdulharam Kaniki.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akisindikizwa  na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser (kushoto) pamoja na Maafisa wengine wa ubalozi huo, mara baada ya kumaliza shughuli ya Marekani ya kuikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment