WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Monday, 7 March 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blasser (katikati) pamoja na Kaimu Naibu Balozi wa Marekani, Vicent D’Spera, kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Kaimu Balozi huyo nchini. Viongozi hao wa Ubalozi wa Marekani nchini walimtembelea Naibu Waziri Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blasser (kulia) akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni wakati Kaimu Balozi huyo alipomtembelea Naibu Waziri Masauni ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na Wizara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akifurahi jambo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blasser (katikati) pamoja na Kaimu Naibu Balozi wa Marekani, Vicent D’Spera, baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara na Ofisi ya Kaimu Balozi huyo nchini. Viongozi hao wa Ubalozi wa Marekani nchini walimtembelea Naibu Waziri Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.No comments:

Post a Comment