WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday, 16 March 2016

WAZIRI KITWANGA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA ZANZIBAR, AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI SIKU YA KUPIGA KURA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Brigedi Kamanda wa 101 KV Zanzibar, Brigadia Jenerali, Cylir Mhaiki, kabla ya kufanya mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi, Zanzibar, Ali Abdalla Maalimmosi. Waziri Kitwanga yupo Zanzibar kwa kwa ziara ya kikazi ya kuangalia hali ya uimarishaji wa usalama visiwani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar. Waziri Kitwanga aliwataka wakuu hao kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unazidi kuimarishwa katika maeneo mbalimbali ya visiwani humo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi mjini humo.

Brigedi Kamanda wa 101 KV Zanzibar, Brigadia Jenerali, Cylir Mhaiki (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati wa kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar na Waziri huyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi, Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar mara baada ya kumaliza mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama visiwani humo. Waziri Kitwanga amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi Machi 20, 2016 bila kutishwa na mtu yeyote, na kila mwananchi aondoe hofu siku hiyo kwani vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri kwa ajili ya kuusimamia uchaguzi huo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


No comments:

Post a Comment