Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati),
akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli alipokuwa
anatoa maelezo mafupi jinsi Watendaji wa Idara yake walivyouandaa Mkataba wa
Huduma kwa Mteja ambao Balozi huyo aliuzindua Makao Makuu ya Idara hiyo,
Kurasini, jijini Dar es Salaam. Mkataba huo unalenga kuboresha zaidi huduma
zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano
za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia
Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi.
|
No comments:
Post a Comment