WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday 27 September 2016

MASAUNI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA MJINI GEITA LEO

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliagiza kuwa matuta yote yaliyopo katika barabara kuu yaondolewe na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali yanavyovunja sheria za barabarani. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika Kitaifa mjini Geita, Mhandisi Masauni aliagiza matuta yote yaliyopo katika barabara kuu yaondolewe na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kuondoa ajali ambazo zinasababishwa na madereva wazembe.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yanafanyika Kitaifa katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita, yalipokuwa yanaingia katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuadhimisha wiki hiyo. Masauni katika hotuba yake aliagiza matuta yote yaliyopo katika barabara kuu yaondolewe na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa zawadi ya Kombe la Ushindi wa kwanza Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent, ambaye alishinda nafasi ya kwanza katika uchorani wa picha zinazoonyesha usalama barabarani ambayo zilipambanishwa katika shule za Mkoa wa Dar es Salaam na Geita. Masauni aliyazindua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, ambayo yanafanyika Kitaifa, katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita. Masauni katika hotuba yake aliagiza matuta yote yaliyopo katika barabara kuu yaondolewe na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.
Washiriki wa maonesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki ajali tunataka kuishi salama”. Maadhimishjo hayo yalinduliwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Katika hotuba yake Masauni aliagiza kuwa matuta yote yaliyopo katika barabara kuu nchini yaondolewe na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika Kitaifa katika Viwabya vya CCM Kalangalala mjini Geita. Maadhimisho hayo yalizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia).

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi cheti cha ushiriki, Mwakilishi wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Amanda Walter.  toa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliagiza kuwa matuta yote yaliyopo katika barabara kuu yaondolewe na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment