Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (aliyembeba mtoto), Mkuu wa Mkoa
wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kulia kwa Masauni), pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani wakiwa katika picha ya pamoja na Watoto Yatima wa Kituo cha
Moyo wa Huruma cha mjini Geita, wakati Mwenyekiti huyo wa Baraza pamoja na
wajumbe wake kukitembelea kituo hicho na kukabidhi misaada mbalimbali. Tukio
hilo lilifanyika mara baada ya Masauni kuizindua Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani ambayo inaadhimishwa Kitaifa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Masauni
awaomba Watanzania kuchangia vituo vya watoto yatima
Na Mwandishi Wetu (MOHA)
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa
la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni amewaomba Watanzania kuweka
utamaduni wa kuvisaidia vituo vya watoto yatima nchini ili kuwasaidia watoto
hao ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Masauni
alisema hayo mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali katika Kituo cha Watoto
Yatima cha Moyo wa Huruma ambacho kinasimamiwa na Kanisa Katoliki mjini Geita.
Naibu
Waziri huyo ambaye yupo mjini humo kwa ajili ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa
Usalama ambayo aliizindua jana Septemba 26 katika Viwanja vya CCM Kalangalala
ambapo inafanyika kitaifa mjini humo.
Masauni
aliwaongoza Wajumbe wa Baraza la Taifa kukusanya fedha taslimu shilingi 1,119,000
kituoni hapo ambapo licha ya fedha hizo Baraza hilo lilitoa misaada mbalimbali ikiwemo
mchele gunia moja, kilo 50 za sukari, dumu la mafupta ya kupikia, sabuni Katoni
11 pamoja na fulana 100, alisema lazima Watanzania tuweke utamaduni wa
kuvichangia vituo vya watoto yatima.
“Natoa
pongezi kwa uongozi wa Kanisa Katoliki kwa kukisimamia kituo hiki, kuishi na
watoto wetu, kuwahudumia vizuri, kwa kweli hili linapaswa kupongezwa. Tupo hapa
Geita kwa ajili ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani lakini
tumeguswa na kuamua kutoa michango mbalimbali kwa kituo hiki, na tunawataka
Watanzania pia waweke utamaduni huu wa kuvisaidia vituo hivi katika sehemu mbalimbali
waliopo nchini,” alisema Masauni.
Masauni
aliongeza kuwa, Serikali ya Rais John Magufuli ipo kwa ajili ya kuwasaidia
Watanzania wote, kama mnavyoona katika elimu imeweka kipaumbele ili watoto wetu
waweze kusoma katika mazingira mazuri.
Kwa
upande wake Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna,
Mohamed Mpinga alitoa pongezi kwa Naibu Waziri Masauni kwakuwaongoza kutoa
misaada hiyo kwa kituo hicho.
“Mwenyekiti
wa Baraza ametuonyesha njia, ametuongoza na kuweza kufanikisha zoezi hili la
uchangiaji, tunamshukuru sana kwa uamuzi huo wa busara wenye nia njema ya
kuwasaidia watoto wetu.” Alisema Mpinga.
Aidha,
Mlezi wa Kituo hicho, Sista Adalbera Mukure alimshukuru Masauni pamoja na
Wajumbe hao kwa moyo wao wa kukichangia kituo hicho, pia aliishukuru Serikali
ya Awamu ya Tano kwa kufanya mambo mengi yanayoonekana.
“Tunafuraha
sana kwa ujio wenu, tunashukuru sana kwa misaada mbalimbali mlioitoa, na pia
tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya mambo mengi yanayoonekana,
sisi tunasaidia serikali hii kwa sala zetu, hatupo katika siasa,” alisema Sista
Mukure.
|
No comments:
Post a Comment