WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 27 September 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI, MJINI GEITA LEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unafanyika leo katika Ukumbi wa wa Mikutano wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita.
Sehemu ya Wadau na Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita.
Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya ajali za barabarani nchini katika mkutano wa Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini. Mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad Masauni, na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa wa Mikutano wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment