WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday 17 August 2016

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI, DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akizungumza na Balozi wa Israeli nchini, Yahel Vilan (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Israel na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Israeli nchini, Yahel Vilan alipokuwa akizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimkaribisha Balozi wa Israeli nchini, Yahel Vilan (kushoto), ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati Israel na Tanzania. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:

Post a Comment