Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari
mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani
nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza
mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini
itatolewa. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye
pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo
umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
|
No comments:
Post a Comment