WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Saturday 15 July 2017

MASAUNI ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUFUNGUA KITUO MAKAZI YA KABILA LA WAHAZABE

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay (wapili kulia) wakicheza ngoma ya Wabarbaig/Watatoga kabla ya Masauni kuzungumza na mamia ya wananchi wa Kabila maarufu la Wahazabe na makabila mengine yaliyopo katika Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi mkoani humo, kujenga Kituo cha Polisi kwa uharaka ili jamii hiyo ambayo inaishi pembezoni mwa mji wa Mbulu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi wa Kabila maarufu la Wahazabe na makabila mengine yaliyopo katika Bonde la Yueda Chini, Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi mkoani humo, kujenga Kituo cha Polisi kwa uharaka ili jamii hiyo iweze kupata ulinzi wa kutosha katika eneo hilo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akijadiliana na maafisa wa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara pamoja na watendaji mbalimbali wa wilaya hiyo, ndani ya jengo la mifugo lililopo Yaeda Chini katika makazi ya Wahazabe, ambalo linatarajiwa kufunguliwa Kituo cha Polisi. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara (RPC), Francis Massawe, na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Massay.
Wananchi wakimshangilia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati alipowatangazia kufunguliwa Kituo cha Polisi hivi karibuni katika Kijiji cha Bonde la Yueda Chini, lililopo wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



No comments:

Post a Comment