WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Saturday, 15 July 2017

MASAUNI APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA KWA AJILI YA CHUO CHA UHAMIAJI CHA KIKANDA (TRITA), MJINI MOSHI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akipokelewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala, wakati kiongozi huyo alipokua anawasili Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), mjini Moshi kwa ajili ya kukabidhiwa vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (kulia) wakipokea moja ya kompyuta kutoka kwa Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (wapili kushoto) katika hafla ya makabidhiano ya vifaa msaada vya Tehama vyenye thamani ya shilingi milioni 33 vilivyotolewa na Ubalozi huo kwaajili ya kukisaidia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo mjini Moshi. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Maurice Kitinusa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia-waliosimama) akishuhudia Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala walipokua wakitia saini Mkataba wa Makabidhiano wa msaada wa vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), kilichopo mjini Moshi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (kushoto), Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (aliyevaa saa) pamoja na maafisa wengine wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), Mkaguzi wa Uhamiaji, Zawadi Chazuka alipokua anawaonyesha kifaa cha kuangalia alama au maandishi ambayo hayawezi onekana kwa macho ya kawaida mpaka kifaa hicho kitumike. Ubalozi wa China ulitoa msaada wa vifaa vya Tehama vyenye thamani ya shilingi milioni 33 kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho kilichopo mjini Moshi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (watatu kushoto), Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (watatu kulia), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa Uhamiaji na Ujumbe kutoka China mara baada ya Balozi wa China kutoa msaada wa vifaa vya Tehama kwa ajili ya matumizi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo mjini Moshi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment