WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 13 May 2014

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YATARAJIA KUTUMIA SHILINGI BILIONI 955.934 KATIKA MWAKA WA FEDHA 2014/2015


Waziri wa Mambo ya Ndani yaNchi, Mathias Chikawe akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo katika Kikao cha Pili cha Baraza hilo kilichofanyika Giraffe Hotel jijini Dar es Salaam leo. Katika kikao hicho, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imependekeza kutumia Shilingi Bilioni 955.934 katika Mwaka wa Fedha 2014/2015. Piha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, Waziri wa wizara hiyo, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku moja unaofanyika katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (kulia) na Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo, JenithaNdone wakiimba nyimbo ya mshikamo daima katika Kikao cha Baraza la Wfanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akimkabidhi Staford Busumbiro (kushoto) Shiingi milioni Mbili kwa niaba ya Haidhuru Kita kwa kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika mwaka 2014. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil na Jenitha Ndone, Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  

Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2014/15 kwa Wajumbe wa wizara hiyo katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe, jijini Dar es Salaam. Katika Mwaka wa Fedha wa 2014/2015 wizara hiyo inatarajia kutumia Shilingi Bilioni 955.934. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia-waliokaa). Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (wapili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa idara wa wizara hiyo na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kufunguliwa Kikao cha siku moja cha Baraza hilo kilichofanyika katika Hoteli ya Giraffe, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:

Post a Comment