Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia),
akimkabidhi jezi za timu sita za mpira wa miguu Afisa Mtendaji wa Kata ya
Nditi, Patrick Mwasambungu kwa ajili ya kuzikabidhi timu hizo zilizopo katika
Kata hiyo katika Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe pia alitoa
mabati 100 kwa ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Mbunge
huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza
na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto),
akikiangalia kifusi cha mchanga kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya
Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika
ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa.
Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni mwake kwa ajili ya kufanya ziara ya
kuzungumza na viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto),
akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mnerongongo ambayo ipo katika hatua ya
mwisho kukamilika ujenzi wake. Katika ujenzi wa ofisi hiyo, Waziri Chikawe
alitoa mabati 100 ambayo tayari yameezekwa. Mbunge huyo wa Nachingwea yupo jimboni
akifanya ziara ya kuzungumza na viongozi
wa CCM katika Kata za Wilaya za Nachingwea mkoani Lindi.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia),
akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Nditi, Wajumbe wa
Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la
Wazee katika Kata hiyo ya Nditi wakati alipofanya ziara katika kata hiyo
iliyopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe alitoa mabati 100 kwa
ajili ya ujenzi ya Ofisi Kuu ya CCM katika Kata hiyo ya Nditi. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment