Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe,
akifurahi na Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha
Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi kabla ya kufuturu nao futari maalum
aliyoiandaa kwa ajili ya watoto hao zaidi ya 80 ambao wanalelewa katika kituo
hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akijiandaa kufuturu na
Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini
Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari maalum kwa ajili ya
watoto hao zaidi ya 80 ambao wanalelewa katika kituo hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati), akizungumza jambo na
Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Abdul Mpakate (watatu kulia) wakati wa kufuturu
futari maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Watoto Yatima na Waishio katika
Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi. Waziri
Chikawe aliandaa futari hiyo kwa watoto zaidi ya 80 wanaolelewa katika kituo
hicho.
Shekhe Mkuu wa Wilaya
ya Nachingwea, Abdul Mpakate akitoa dua la kumshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto),
kwa kuandaa futari maalum kwa ajili ya Watoto Yatima na Waishio katika
Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi. Waziri
Chikawe aliandaa futari hiyo kwa watoto zaidi ya 80 wanaolelewa katika kituo
hicho. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment