WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Friday, 18 July 2014

WAZIRI CHIKAWE ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU JIMBONI KWAKE NACHINGWEA LEO

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe  (kushoto), akiupokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Chiola, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya Mwenge huo kumaliza kukimbizwa katika Wilaya Ruangwa. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru uliotoka Wilaya ya Ruangwa na kuingia Wilaya ya Nachingwea. Wapili Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo ambaye ndio aliyekabidhiwa rasmi Mwenge huo kutoka Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (kulia) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chiola (hawapo pichani) baada ya kufungua Mradi wa Nyumba ya Mganga katika  Kijiji hicho kilichopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (aliyebeba ndoo ya maji) akishangiliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo pamoja na wananchi baada ya kubeba ndoo ya maji baada ya kufungua mradi wa maji katika Kijiji cha Mituguru, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Wapili kulia ni  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo. Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” umengia katika wilaya hiyo ambapo unatarajiwa kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungu, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya kukabidhi Bajaj kwa walemavu na Pikipiki kwa watendaji wa Wilaya na Kata mbalimbali katika wilaaya hiyo zikiwa ni kwa shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akiwasalimia wapiga kura wake wa Kijiji cha Ikungu wakati wa ukimbizaji wa Mwenge wa Uhuru katika Jimbo lake la Nachingwea.  Waziri Chikawe alimshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda pamoja na timu yake kwa kuzindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.




No comments:

Post a Comment