WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 15 July 2014

WAZIRI CHIKAWE, BALOZI WA MAREKANI WAJADILIANA MASUALA YA USHIRIKIANO JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe na Balozi huyo walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na Wizara. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini. Balozi Childress alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment