WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tuesday, 15 July 2014

MWAKILISHI MKUU WA KANDA ICRC AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE DAR LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) katika nchi za Djibouti, Kenya na Tanzania, Thierry Meyrat (wapili kulia) wakati Mkuu huyo pamoja na ujumbe wake walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya kamati hiyo na Wizara. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. Kushoto ni Profesa Umesh Kadam, Mwanasheria ICRC katika kanda hiyo na Martha Kassele, Ofisa wa Program ICRC. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mwakilishi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) katika nchi za Djibouti, Kenya na Tanzania, Thierry Meyrat (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya kamati hiyo na Wizara. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimshukuru Mwakilishi Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) katika nchi ya Djibouti, Kenya na Tanzania, Thierry Meyrat kwa kumtembelea ofisini kwake na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na ICRC. Kulia aliyekaa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. Kushoto ni Profesa Umesh Kadam, Mwanasheria ICRC katika kanda hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment