WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Thursday 10 July 2014

SERIKALI YA JAPAN YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WAKIMBIZI NCHINI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea msaada wa chakula kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma chenye thamani ya Dola ya Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3 Bilioni, ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan. Waziri Chikawe alipokea msaada huo na kumkabidhi Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa WFP, Regan, Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha na Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akipokea galoni ya mafuta ya kula kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto) ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya chakula cha msaada kwa ajili ya Wakimbizi kilichotolewa na Serikali ya Japan. Kulia ni Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan akipokea msaada huo kutoka kwa Waziri Chikawe ambao una thamani ya Dola za Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3 bilioni katika tukio la makabidhiano lililofanyika jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimshukuru Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto) kwa msaada wa chakula wenye thamani ya Dola za Marekani 1.4 milioni ambao ni sawa na Shilingi 2.3 Bilioni ambao Serikali yake imetoa kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan ambaye alikabidhiwa msaada huo baada ya Waziri Chikawe kuupokea katika sherehe fupi ya makabidhiano iliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment