WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Sunday 14 September 2014

WAZIRI CHIKAWE ATEMBELEA KITUO CHA MPITO CHA WAKIMBIZI MJINI KIGOMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiwa ndani ya moja ya nyumba za Wakimbizi waliopo katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma. Katika nyumba hiyo Waziri Chikawe alizungumza na familia ya mkimbizi kutoka nchini Kongo (kushoto) wanaoishi katika nyumba hiyo. Waziri Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Wapili kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Kituo hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi  ya muda ya ukimbizi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiangalia jiko ambalo linatumika kupikia chakula cha wakimbizi katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Waziri Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Kituo hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi  ya muda ya ukimbizi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimsalimia mkimbizi kutoka nchini Kongo aliopo katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma. Waziri Chikawe na maafisa wake wapo mkoani Kigoma kwa ajili ya ziara ya kikazi. Kituo hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi  ya muda ya ukimbizi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akiwasalimia waimba kwaya wakimbizi kutoka nchini Kongo waliopo katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma. Waimba kwaya hao walimpokea Waziri Chikawe kwa nyimbo mbalimbali wakati alipotembelea Kituo hicho cha mpito.  Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Waziri Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Kituo hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi  ya muda ya ukimbizi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment