WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Sunday, 14 September 2014

WAZIRI CHIKAWE ATUA KIGOMA, AKUTANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe katika ofisi za Mkoa huo zilizopo mjini Kigoma wakati Waziri Chikawe na maafisa wake walipofanya ziara ya kikazi katika mkoa huo. Waziri Chikawe alikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya usalama katika wilaya zote za mkoa huo. Waziri Chikawe katika ziara yake hiyo, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya akizungumza  katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Ofisi yake. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ambaye pia alishiriki katika kikao hicho kilichokuwa kinajadili masuala mbalimbali ya usalama mkoani Kigoma. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani hum leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kikao kilichoitishwa kwa ajili yake, na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya. Katika kikao hicho kilichofayika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi za Mkoa wa Kigoma, Waziri na Kamati hiyo walijadiliana masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani humo leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na  Kamati hiyo ya mkoa, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma. Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya. Waziri Chikawe pamoja na kamati hiyo walifanya kikao kilichofayika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi za Mkoa wa Kigoma, wakijadiliana masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama ndani ya mkoa huo. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani humo leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na  Kamati hiyo, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment